Diamond Platnumz Moyo Lyrics

Diamond Platnumz Moyo Lyrics

Verse 1

Pole pole pole,
Pole pole,
Moyo wangu,
Masikini pole,
Pole mtima wangu.

Haikuwa dhamira,
Haikuwa kusudi langu,
Haikuwa dhumuni waala,
Haikuwa malengo yangu.

Ila tuseme,
Labda moyo,
Pengine sio,
Ridhiki.

Maana,
Nimejitahidi sana,
Malengo hayafiki.
Kama kuswali,
Naswali sana,
Mpaka sunna za usiku.

Kazi nimetafuta sana,
Ila siambulii kitu.
Sitaki kukufuru Mungu,
Sababu najua ni mapito.
Japo inakatisha tamaa,
Ila siku yangu ipo.

Chorus

Moyo, usiumie,
Moyooo, ni mapito,
Ohh moyo,
Haya yote,
Mitihani na yana mwisho.

Moyo wangu, moyo,
Usiumie,
Moyooo, ni mapito,
Ohh moyo,
Haya yote,
Mitihani na yana mwisho.

(Instrumental)

Verse 2

Penzi maua,
Pesa mbolea.
Hata shemeji yako,
Ana mengi ila,
Hawezi ongea.

Moyo,
Najitahidi jiepusha vya watu,
Ni majaribu aah,
Japo nna shida,
Ila naepuka tamaa.

Moyo,
Nlitamani siku moja,
Na mimi nimjengee mama,
Ila ndo vile tu umasikini,
Mipango inakwama.

Hua naumia,
Watoto shuleni,
Wakifukuzwa ada.
Najiona mjinga,
Yani sio bora baba.

Sitaki kukufuru Mungu,
Najua ni mapito.
Maana riziki mafungu,
Nami langu siku lipo.

Chorus

Moyo, usiumie,
Moyooo, ni mapito,
Ohh moyo,
Haya yote,
Mitihani na yana mwisho.

Moyo, usiumie,
Moyooo, ni mapito,
Ohh moyo,
Haya yote,
Mitihani na yana mwisho.

Recommended:

  1. Harmonize Furaha Lyrics
  2. Jux Si Mimi Lyrics
  3. Killy Niokoe Lyrics
  4. Vanillah Ni Kwa Muda Lyrics
  5. Kusah Blessing Lyrics